MWIGIZAJI BALAYA {The Prostitute Actor} Sehemu Ya 1 Mtunzi..... MoonBoy Simu No. +255714419487 WhatsApp Ilipoishia Jana →↓↓↓↓↠Sasa siku hio ilikua ni siku ya kikao cha usiku, baina ya watu wote.. Yaani familia nzima na alioitisha mkutano huo ni dada batuli kana kwamba ndio anataka kuliongelea lile swala la mimi kwenda Dar es Salaam... Na mimi nilikuepo kwa pembeni nimewategea tu skio langu,... "ndugu wazazi wangu wapendwa... Leo nimewaita hapa nina ombi moja kwenu japo sio la muhimu sana jwenu.... Aahhh kama mnavyojua kazi zangu mimi ni uigizaji, na katika tasnia yetu hua hatuweki mtu ilimladi mtu bali tunaangalia kipaji cha mtu ili aweze kukava ile nafasi husika, na nimeona kuna nafasi sheby anaiweza...." Kila mmoja alianza kutoa macho huku mzee mwenyewe akiuliza, kua "Uu..u..uu...unasemaje we mtoto" "baba na ndugu zangu wote... Nataka niondoke na sheby, tukaishi Dar es Salaam ili akijue kipaji chake... " Mara mzee akaamka kwa hasira huku ak...