Skip to main content

KIJAKAZI WA KIUME Sehemu Ya 1

KIJAKAZI WA KIUME 1

sehemu ya 1

MTUNZI: MoonBoy

SIMU +255714419487 whatsapp

KIJAKAZI WA KIUME ni kijana mmoja aishie MANYARA WILAYA YA KITETO VIJIJINI HUKO KATIKA MTAA UNAOITWA KIBAYA. kijana huyo aitwae SHARBINY au unaweza kumuita SHEBY yaani ni nusu ya jina lake. kijana sheby ni kijana mpole mwenye heshma na adabu na kumueshim kila mtu alie mbele yake. lakini kija huyo alikua akiishi maisha magumu mno tena magumu zaidi ya magumu. kijana sheby alitamani kusoma hadi vitabu vimkimbie  lakini kutokana na maisha alionayo basi aliweza kuishia DARASA LA SABA. kijana sheby ni kijana ambae hana wazazi  yaani ni yatima na wazazi wake walifariki toka yeye akiwa mtoto mdogo sana. kwaio hajui hata sura za wazazi wake zikoje. kijana sheby alitamani hata kujua wazazi wake waliuwawa na nini lakini atamuuliza nani na kijana huyu alikua akiishi na bibi ake wa upande wa baba. na kila anapomuuliza kuhusu swala la wazazi wake  bibi yeye anasema hajui na wala hawajui tena maana ni muda sasa. basi sheby alibaki kukaa bila wazazi siku zote na miaka yote anachojua tu ni kwamba ana mjomba wake ambae yupo mjini arusha aitwae said. sheby alikua ni mkulima mzuri sana wa mazao mbali mbali hususani kama mahindi Na majirani na watu wote walimpenda kijana huyo kutokana na kuchapa kazi vizuri. na hata mabint pia walikua wakijikwaa sana kutokana na uchapakazi wake. UNAWEZA UKAULIZA KUA KWANI SHEBY ALIKUA HENSAMBOY? MIMI NITAKUJIBU HAPANA. KWANI MJINI NDIO WANAPENDA VIJANA MAHENSAMBOY BALI KIJIJINI WANAPENDA VIJANA WACHAPA KAZI NA WENYE NGUVU. ILA KIJANA HUYO HAKUA HENSAM BALI ALIKUA ANAKAMVUTO KA MWILI YAANI ANA KABODI FLANI HIVI KALIKOJAZIA VIZURI. MAANA ANAPENDAGA KUKIMBIA KIMBIA KILA SUBUHI NA PUSHAPU KIDOGO. SASA USIJE UKASEMA KUA SHEBY NI HENSAM.. HAPANA BALI SHEBY MCHAPA KAZI MZURI SANA
basi bwana.. sheby alikua ni kijana mmoja mpole kuliko wapole wote hapa duniani. kana kwamba kama kungelikua na mashindano ya kumtafuta mtu mpole duniani basi sheby angenyakua taji la upole dunia nzima. sheby ni kijana anaemueshim kila mtu au kila lika. yaani kosa ni lako lakini atakuomba msamaha yeye badala ya wewe mwenye kosa. sheby alipendwa na kila mtu kutokana na ukarimu wake pia sheby alikua mcheshi yaani sifa zote nzuri yeye anazo... yote tisa   kumi chidi alikua ni muislamu mzuri sana yaani hakosa swala hata moja afu anajua dini vibaya mno.. chidi alikua ni mchunga ng'ombe na mbuzi za watu maana akikaa tu nyumbani atamlisha nini bibi yake. na bibi yake hawezi kuhangaika sana japo ana nguvu kidogo. bibi ake sheby wa upande wa baba ukimuangalia vizuri utagundua kua si mkongwe saana kama ana umri wa miaka  58 hadi 65 ivi kwaio si mkongwe sana. na hata ukihesabu umri wake basi utapata jibu kua hata wazazi wa sheby baasi si wakubwa sana labda wawe na umri wa miaka kama 38 au 40 hivi maana sheby yeye ana miaka 20 au 21 hivi maana aliambiwa tu na bibi ake kua ana umri huo. na sheby alikua akimuuliza bibi ake kua   je bibi na babu wa upande wa mama wako wapi?? bibi anasema wamefariki dunia muda mrefu tu. na story alizopewa na wamama wanaompenda sheby walikua wakimuadisia story ya wazazi wake jinsi walivyokutana kua walikutana shuleni na wakajikuta wamepeana uja uzito ambao ndio wewe na kipindi hicho kulikua na sheria kali ya mwanafunzi yeyote atakaebeba/bebesha mimba atahukumiwa miaka kadhaa jela au asubiriwe mtoto azaliwe kisha auwawe mtoto huyo ili wazazi wake waendelee na masomo. kwaio kutokana na sheria zile wazazi wa sheby hawakukubali mtoto wao auwawe mbele ya macho yao. na ndio ilipofika siku ya kujifungu katika hospitali moja iitwayo KIBAYA HOSPITAL mama yako alijifungua mtoto wa kiume ambae ni wewe na wakati huo anajifungua nje kulikua na askari kadha wa kumlinda mama yako na baba yako ili msitoroke. ndipo mama ake sheby alipomaliza tu kujifungu alimpa jina pale pale kitandani. kisha akamshika mkono mume wake na kutoka nae nje wakati huo sheby kaachwa kitandani sasa mama sheby na mumewe au mchumba wake walipofika nje waliwaambia wale askari kuoa    "kuliko auwawe mtoto wetu ni bora tufe sisi na kuliko mutuu ninyi maaskari bora tukajitungike porini tuliwe na wanyama"





Na ndipo walipochukua jukumu la kukimbia na kuelekea maporini kujiua na toka hapo hajaonekana mzazi wa sheby hata mmoja.. ndipo akalelewa na bibi ake mpaka sasa.
sheby alikua ni mtu anaependa shule lakini kaishia la saba kutokana na hali ngumu ya maisha.. maana wazazi wake waliishia darasa la sita kwa kubebeshana mimba.. kijana sheby alikua akifanya kazi nyingi sana ambazo hata mtu mzima hawezi kabisa maana
alikua akitoka asubuhi saa 11 alikua anawahi kulima mashamba ya watu ili apate pesa  kisha inapofika mida ya saa 3 asubuhi anakwenda shambani kwake na inapofika saa 6  anakwenda kuchunga mifugo ya watu ili apate pesa ya kumkidhi mahitaji yake.. sheby ni kijana anaependa kujisomea sana lakini cha ajabu geto lake limejaa vitabu vya mapenzi tu.. na ni vya kiswahili maana kingereza hajui hata tone zaidi ya neno YES au NO lakini kiswahili kidoogo anakijua kukisoma na kuandika maana kama unavojua shule za vijijini uspokua makini basi utatoka ziro.. basi kijana sheby kila akilipwa pesa ya machugaji yeye asilimia nyingi hununua vitabu vya mapenzi
SASA TWENDE NAYO  HUKO ILIKUA NI UTAMBULISHO TU ILI UJUE MWANZO WA MAISHA YA   SASA SONGA NAYO....
Siku moja nilikua natoka machungani na ilikua ni mwisho wa mwezi yaani ilikua ni siku ya malipo yangu kwa kazi ya uchungaji ng'ombe na mbuzi. na kwa kawaida naendaga mida ya jioni saa 1 hivi. basi nikaanza kupitia pesa zangu kwenye nyumba moja hivi ya mdada
"hodi? hodi? hodi wenyewe?"
"karibuu"
"asante"
"naniii?"
"ni mimi mchungaji"
"aahh  enhee unasemaje?"
"nimekuja kupitia hela yangu"
"ni sh ngapi?"
"ni elf 3 tu"
"heee we mtoto elf 3 kwa siku nani atakupa?"
"sii kwa siku mamaa"
"eeh kwa wiki au?"
"hapana ni kwa mwezi"
yaani kila nyumba yenye mfugo basi ni elf 3 kwa mwezi
"hee we mtoto hebu nikuone ivi utakua mzima kweli wewe?"
"kwanini?"
"elf 3 kwa mwezi?"
"basi elf 2000 kama hio ni kubwa"
"hebu ingia mpaka ndani we kijana"
basi nikaingia mpaka ndani na kumuona huyo mama mwenyewe.. hata hivyo mama mwenyewe alikua ni mgeni yaani alitoka mjini na ndio maana alikua anauliza maswali mengi sana kuusu pesa.
"shkamo"
"marahaba ujambo?"
"sijambo mama"
"wewe ndio mchungaji?"
"ndio mama"
"jamani mbona hufananii kabisa"
"ndio kazi yangu mama"
"jamani pole?"
"asante sana"
mara akatokea mwenyeji wa nyumba hio
"kumbe ndio maana nasikia harufu ya mbuzi mbuzi kumbe ni huyu mchungaji?"
yule mama mgeni alimuangalia vibaya huyu ndugu yake
"eti kijana unaitwa nani"
"unamuuliza wanini bwana mpe hela yake atutolee harufu apa"
"we mama jeni kua na huruma basi"
"bwaanae nipishe uko"
yule mama mgeni alitoa noti ya elf 10 na kunipa mimi
"hee unampa elf 10? yanini yote hio au kakuambia anatudai?"
"hapana nimeamua kumpa tu"
"we mchungaji we?"
aliniita huyu mama jeni
"naam"
"hio ni miezi mitatu sawa?"
"sawa"
"nawe unakubali tu si umuambie nimepewa tu"
"aahh wacha tu nifanye anavotaka maana wewe utarudi mjoni kwenu afu huyu ataninyima pesa zangu endapo nitakufatiliza wewe"
"basi usijali mwanangu  hebu twende nikutoe"
baasi mama alinitoa hadi nje kisha akaniongezea elf 10 nyingine
kisha akaniambia kitu fulani kwa kuninong'oneza
Lakini kitu chenyewe kilinipa mawazo pale pale kutokana na jinsi nilivyo. sasa nikajikuta nimeduaa
"we kijana? we kijana? we mtoto usije ukanifia bure hapa mbona huongei?"
nilibaki kimya nikitafakari jambo aliloniambia

JE NI JAMBO GANI HILO??

USIKOSE KESHO MIDA KAMA HII

LIKE/ COMENT...

Comments

Popular posts from this blog

JAMANI ANKO Sehemu Ya 1

JAMANI ANKO Sehemu Ya 1 MTUNZI: George Iron Mosenya SIMU:0655727325 Nilitamani muda wa vipindi darasani umalizike ili iweze kutimiza ahadi niliyokuwa naisubiri kwa siku nyingi. Mwalimu alikuwa akifundisha lakini ni kama nilikuwa sielewi wala sisikii alichokuwa anaelezea. Mawazo yangu yote yalikuwa kwa Madam Jesca. Siku hiyo nilijisemea kuwa iwe isiwe lazima nimweleze ukweli na ikibidi siku hiyo hiyo yatimie ninayoyawaza kila kukicha. Madam Jesca alikuwa ni mwalimu aliyekuwa akitufundisha kwa muda tu baada ya kuwa amemaliza kidato cha sita. Wakati huo sisi tulikuwa kidato cha nne. Somo alilokuwa akitufundisha ni Kiswahili. Hatimaye mwalimu akatoka na baada ya nusu saa nikaondoka kuelekea nyumbani kwa madam Jesca. Niliingia baada ya kuwa nimegonga hodi. “We Joshua mbona muda wa vipindi hivi we umekuja huku..” aliniuliza huku macho yake yakionyesha mshangao wa waziwazi. Kanga yake aliyovaa ilikuwa imelowana na hivyo kusababisha niuone mstari wa chupi. Na kama hiyo haitoshi madam Jesca...

MUUZA CHIPSI Sehemu Ya 1

MUUZA CHIPSI (MKE WA KAKA) Sehemu Ya 1 Mtunzi..... MoonBoy Simu No. +255714419487 WhatsApp www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/ INAPOANZIA RASMIIII Jamani Simulizi hii, sio moja, bali zipo simulizi mbili ndani ya moja... Kuna simulizi yangu moja iliitwa MKE WA KAKA hio simulizi inaendana na simulizi hii ya MUUZA CHIPSI, hivyo sikutaka simulizi zangu ziwe zinajirudia, hivyo nimeiweka sehemu moja zote mbili, mana stori za simulizi hizi zinaenda.. Hivyo ukisoma jua kua unasoma simulizi mbili ndani ya moja... Ila simulizi halisi ni MUUZA CHIPSI ikifuatiwa na MKE WA KAKA ambayo nayo ipo humu humu ndani,.   Na utaijua hapo itakapoanzia rasmi lakini mwanzo wa zote ndio, lakini pia MKE WA KAKA ina mwanzo wake huko mbele, hivyo nayo inaanzia hapa hapa....... Sasa ole wako uikose staki maswali mengi mana umekosa uhondo mwenyewe... Hivyo msije mkashangaa mke wa kaka kawa MUUZA CHIPSI.... ______________________________________ MUUZA CHIPSI Ni simulizi inay...

SECONDARY SCHOOL Sehemu Ya 1

SECONDARY SCHOOL Sehemu Ya 1 Mtunzi..... MoonBoy Simu No. +255714419487 WhatsApp Inapoanzia Rasmiiii STORY HII INAITWA SECONDARY SCHOOL AU KWA KISWAHILI NI ( SHULE YA UPILI )..... KWAHIO PIA WAWEZA KUIITA HIVYO TU BASI Story hiii mimi ni mtoto wa kitajiri ile mbaya... na wakiume nipo mimi mwenyewe na nina dada zangu wawili wenye asili ya kiarabu. kwani mama yangu yeye pia ana asili ya kiarabu..... Ninae dada yangu ambae ana umri wa miaka 25 huyo ni wa kwanza na keshamaliza shule muda tu... kisha ninae dada yangu mwingine ambae tumefuatana.. yeye ana umri wa miaka 22 na yeye bado yupo kidato cha 4... afu anafatiwa na mimi kidume sharbiny rashidy mwenye umri wa miaka 20 na yupo kidato cha 3.... familia yetu ilikua ni familia ya kitajiri sana yaani tulikua ni matajiri waliopindukia.... Ila katika watoto wote wa mzee rashidy mimi peke yangu ndio nilikua nina rangi tofauti na dada zangu wote. Ila nyumba yetu imezungukwa na wafanyakazi wengi mno. kama kwa raisi vile kumbe ni kwa mtu tu wa ka...