Skip to main content

MTOTO WA HAYATI Sehemu Ya 1

MTOTO WA HAYATI

Sehemu Ya 1

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp


SIMULIZI HII INAMHUSU KIJANA MMOJA AMBAE ALIISHI NA WAZAZI WAKE KATIKA MAISHA MAZURI NA YENYE FURAHA, LAKINI KADRI MAISHA YANAVYOZIDI KWENDA, NA WAZAZI WAKE NA HUPOTEZA MAISHA KAMA KAWAIDA, WAZAZI WALIACHA MALI NYINGI KWA AJILI YA MTOTO WAO HUYO MMOJA TU KAMA WA DAWA, LAKINI KUMBE NDUGU WA FAMILIA HIO HAWAKUA WAKIHITAJI UWEPO WA FAMILIA ILE IKIENDELEA KUISHI KWA FURAHA NA UPENDO, MTOTO YULE ALIZURUMIWA MALI ZILE NA NDUGU WA MAMA YAKE, YAANI BABA AU MAMA WADOGO WA UPANDE WA MAMA YAKE, MTOTO ALIISHI KWA SHIDA NA TABU KATIKA NYUMBA HIO, HUKU AKIWA KAMA MFANYAKAZI KATIKO NYUMBA HIO, NA MWISHO WA SIKU WALIAMUA KUMFUKUZA MTOTO YULE......

JE UNAJUA NINI KILIENDELEA BAADA YA KUFUKUZWA?.....  USIKOSE HATA KIPANDE KIMOJA CHA SIMULIZI HIII....  ILA KAMA UNA ROHO NYEPESI USIISOME MAANA INASIKITISHA SANA,

TWENDE KAZI, NA HAPA NDIPO INAPOANZIA RASMI SIMULIZI HIII



Ikiwa ni mwaka 1999 nikiwa mtoto mdogo mwenye umri wa miaka minne, maana nilizaliwa mwaka 1995, Nilikua nikitoka shule ya vidudu, almaarufu kama NURSARY SCHOOL, wazazi wangu walikua wakinipenda sana tena kwa uzuri ni kwamba nilikua nao wote, maisha kwetu yalikua ni mazuri kiasi kwamba baba alikua ana mkoko wake wa kutembelea, huku mama akifanya biashara ya kuuza nguo katika duka lake lililopo maeneo ya stendi jijini arusha, Kama kawaida mama yangu aliitwa MWAJABU na baba yangu aliitwa RASHIDY na mimi mwenyewe niliitwa SHARBINY au ukipenda niite SHEBY,.....  Unaweza kujiuliza sana kwanini napenda kuyatumia hayo majina, ni kwasababu hayo ni majina ya wazazi wangu kabisa, yaani mbali na story zangu, basi hayo ni majina yao na sio ya kutungwa, na hilo jina la sharbiny ni lakwangu kabisa mimi muandishi wa simulizi hizi, hivyo usishangae kila story kuyasoma majina hayo, maana ni majina asilia na ya kweli kabisa......




Siku zilizidi kwenda na hatmae ni miaka mingi imepita mpaka nimemaliza shule ya msingi na sasa ndio naingia kuanza elimu yangu ya secondary kidato cha kwanza katika shule za international, maana wazazi wangu walijiweza kunilipia, maana baba yangu alikua akifanya kazi katika kampuni za kusafirisha wazungu, iitwayo LEOPARD COMPANY LTD ARUSHA kwahio kiukweli maisha yalikua sio mabaya sana,
"sheby?"
"yes dady"
"coming"
Niliitwa na baba yangu sebureni, na baba yangu alikua akiangalia mpira kwenye tv ilio kubwaa ya inchi 40,....  Kipindi hicho nilikua nina umri wa miaka kumi na nne (14), nilikua ni mtu mzima japo nilikua bado sijakomaa kiutu uzima, yaani kwa umri huo kama wewe unaakili basi nilikua bado ni mdogo sana kwani hata kubarehe yenyewe ilikua bado kabisa, na pia kutokana na malezi ambayo nimelelewa na familia yangu, basi ni ngumu sana kujua jua nambo ya kijinga jinga yasio na msingi wowote ule, kwani kawaida nikirudi tu shule hua nakimbilia madrasa au msikitini kusali.....  Simulizi hiii inaendana kidooogo na ile ya SECONDARY SCHOOL ila hii ni balaaa, maana huko mbele mi sisemi ila ukiikosa mi simo




"yes dady"
"umerudi shule mwanangu"
"ndio baba, ila leo hujaleta zawadi dadiii"
"usijali, nitampigia mama yako simu akuletee chipsi kuku na kilo ya nyama, si utamaliza ee"
"ndio, tena nitakula afu sili usiku"
"mmmhhh mtoto muongo wewe, unaweza kumaliza kuku mzima na kilo ya nyama"
"vilete uone navipiga chap chap"
"sawa, tupinge usipomaliza sileti tena zawadi"
"haaaaaaaaa dadiiiii basi simalizi"
"uyoooo ahahahaha nilijua tu"
Nilikua nikifurahi na baba yangu mzazi kana kwamba tunaishi kwa amani na upendo tena kwa furaha ilio ya juu kuliko yeyote yule,....  Sasa we imagen upendo wa baba ni huo je huyo mama itakuaje, yaani ilikua ni familia ya kuigwa na watu wengine kupitia familia,
"vp unataka uangalie katuni zako"
"amna dadii mi nipo chumbani nafanya homework zangu"
"haya bwana"
Kwa upande wa shule kiukweli nilikua kichwa na ndoto zangu ni kuja kua dokta mkubwa katika tanzania hii, hio ndio ilikua ndoto yangu ya baadae,

Maisha yalikua ni mazuri sana juu yangu, kwani wazazi wangu wote walikuepo na walikua wakinipenda sana, maana nilikua nipo peke yangu katika familia yetu,......  Ila siku moja mamkubwa wangu alikuja kutusalimu huku mjini, akitokea kijijini, huyo ni mamkubwa kwa upande wa mama angu,....  Tulimpokea huku tukiwa na furaha juu ya ujio wake huo,  ila siku moja nikiwa naenda msalani kujiseidia, usiku wa saa nane, nilishangaa kuona mtu kakaa nje kwenye kiti na usiku huo, hili lilikua ni jambo geni sana kwangu, niliwaza sana na kujua kua labda huenda akawa ni mama yangu anapunga upepo hapo nje, japo haikua tabia yake ya kupunga upepo mida hio, maana mama yangu anakaaga nje mwisho saa tatu usiku tena ni mpaka kuwe na mwezi ndio anatoka, sasa iweje leo aamke saa hizi,...  Lakini nilipoangalia vizuri, ni kama hakua mwenyewe yaani walikua wapo kama watatu afu kuna mtu wamemzunguka katikati, na siku kwa bahati mbaya hakukua na umeme, walikua kama kuna kitu wanamfanyia huyu mtu waliomueka katikati, ila hakuna niliomuona sura kati yao,

Nilizidi kua na hofu huku nikinyata nyata ili niweze kuwasogelea karibu, lakini wazo langu lililopo kichwani ni kwamba, mimi najua ni baba na mama watakua wanacheza bao na jirani, hivyo nilikua nawamendea ili niwashtue, maana mama na baba wana tabia ya kucheza bao usiku, japo sio usiku mkubwa kama leo hiii, niliendelea kuinama huku nikijificha kwenye gadeni na maua yaliopo hapo, nilikua nahisi baridi sana, kwani nilitoka na boxer tu,......  Lakini nilipofika karibu nilishindwa kuelewa hawa wazazi wangu wanacheza bao gani, mbona sioni hata wakirusha rusha mikono zaidi ya kuona mikono ikiwa juu juu tu.......  Nilijipa moyo kua huenda ni mchezo mpya waliougundua watu hawa, maana si wazee wa zamani hivyo watakua wakijua michezo mingi mno,.....  Nilizidi kusogea mpaka nikakaribia karibu yao huku nikiwa nimejificha kwenye shina la ua moja kubwaaaa, lakini baridi ndio ilikua inanisumbua hivyo nikawa natetemeka sana huku,  nikiwa nataka niwashtue baba na mama kama vile tunacheza kombolela,

Je? Unajua nini kitaendelea?


Itaendelea..... after Tomorrow


KWA STORY ZAIDI BOFYA HAPO CHINI KISHA UNGANA NASI KWA KUGONGA LIKE KWA HIO PAGE YETU →→→↓↓↓

https://www.facebook.com/pages/Moon-vision-Enter/571095712946246?ref=hl

USIKOSE HAPO KESHOKUTWA USIKU... MIDA KAMA HIII HAPA

Comments

  1. Best Casinos in Oklahoma With Bonus Codes 2021
    List of 바카라 Best Casino Sites in Oklahoma With Bonus bet365 배당 Codes 비트코인 시세 사이트 2021 You can easily 벳썸 see why Oklahoma casinos have a 실시간 배팅 good reputation among the top sites for

    ReplyDelete
  2. Baada ya kuwa na uhusiano naye kwa miaka saba, aliachana nami. Nilijaribu kila niwezalo kumrudisha lakini yote yalikuwa bure. Nilitamani arudi vibaya sana kutokana na mapenzi niliyonayo kwake na nilimsihi kwa moyo wangu wote, nilimpa ahadi lakini alikataa. Niliwasiliana na mganga aitwaye DR Dawn, ambaye angeweza kunisaidia kuniroga ili kumrejesha lakini mimi ni mtu ambaye sikuwahi kuamini uchawi, sikuwa na jinsi zaidi ya kujaribu. Nilimtumia barua pepe mganga huyo na akaniambia kwamba hakuna tatizo lolote, kwamba kila kitu kitakuwa sawa baada ya siku mbili na kwamba mpenzi wangu wa zamani angerudi kwangu baada ya siku tatu. Alipiga uchawi na cha kushangaza, siku ya pili, ilikuwa karibu 4:00 PM. Mpenzi wangu wa zamani alinipigia simu, tukasuluhisha tofauti zetu na sasa tuna furaha pamoja. Yeyote anayeweza kuhitaji usaidizi wa mtangazaji huyo anaweza kumtumia barua pepe kwa ( dawnacuna314@gmail.com ) au /WhatsApp kwa: +2349046229159

    Kwa uchawi wa kuungana tena.
    Kwa ujanja wa ujauzito.
    Kushinda bahati nasibu.
    Kushinda kesi mahakamani.
    Mimea ya kutibu, kila aina ya magonjwa kama,
    VVU UKIMWI Kansa malengelenge na zaidi.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

JAMANI ANKO Sehemu Ya 1

JAMANI ANKO Sehemu Ya 1 MTUNZI: George Iron Mosenya SIMU:0655727325 Nilitamani muda wa vipindi darasani umalizike ili iweze kutimiza ahadi niliyokuwa naisubiri kwa siku nyingi. Mwalimu alikuwa akifundisha lakini ni kama nilikuwa sielewi wala sisikii alichokuwa anaelezea. Mawazo yangu yote yalikuwa kwa Madam Jesca. Siku hiyo nilijisemea kuwa iwe isiwe lazima nimweleze ukweli na ikibidi siku hiyo hiyo yatimie ninayoyawaza kila kukicha. Madam Jesca alikuwa ni mwalimu aliyekuwa akitufundisha kwa muda tu baada ya kuwa amemaliza kidato cha sita. Wakati huo sisi tulikuwa kidato cha nne. Somo alilokuwa akitufundisha ni Kiswahili. Hatimaye mwalimu akatoka na baada ya nusu saa nikaondoka kuelekea nyumbani kwa madam Jesca. Niliingia baada ya kuwa nimegonga hodi. “We Joshua mbona muda wa vipindi hivi we umekuja huku..” aliniuliza huku macho yake yakionyesha mshangao wa waziwazi. Kanga yake aliyovaa ilikuwa imelowana na hivyo kusababisha niuone mstari wa chupi. Na kama hiyo haitoshi madam Jesca...

MUUZA CHIPSI Sehemu Ya 1

MUUZA CHIPSI (MKE WA KAKA) Sehemu Ya 1 Mtunzi..... MoonBoy Simu No. +255714419487 WhatsApp www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/ INAPOANZIA RASMIIII Jamani Simulizi hii, sio moja, bali zipo simulizi mbili ndani ya moja... Kuna simulizi yangu moja iliitwa MKE WA KAKA hio simulizi inaendana na simulizi hii ya MUUZA CHIPSI, hivyo sikutaka simulizi zangu ziwe zinajirudia, hivyo nimeiweka sehemu moja zote mbili, mana stori za simulizi hizi zinaenda.. Hivyo ukisoma jua kua unasoma simulizi mbili ndani ya moja... Ila simulizi halisi ni MUUZA CHIPSI ikifuatiwa na MKE WA KAKA ambayo nayo ipo humu humu ndani,.   Na utaijua hapo itakapoanzia rasmi lakini mwanzo wa zote ndio, lakini pia MKE WA KAKA ina mwanzo wake huko mbele, hivyo nayo inaanzia hapa hapa....... Sasa ole wako uikose staki maswali mengi mana umekosa uhondo mwenyewe... Hivyo msije mkashangaa mke wa kaka kawa MUUZA CHIPSI.... ______________________________________ MUUZA CHIPSI Ni simulizi inay...

SECONDARY SCHOOL Sehemu Ya 1

SECONDARY SCHOOL Sehemu Ya 1 Mtunzi..... MoonBoy Simu No. +255714419487 WhatsApp Inapoanzia Rasmiiii STORY HII INAITWA SECONDARY SCHOOL AU KWA KISWAHILI NI ( SHULE YA UPILI )..... KWAHIO PIA WAWEZA KUIITA HIVYO TU BASI Story hiii mimi ni mtoto wa kitajiri ile mbaya... na wakiume nipo mimi mwenyewe na nina dada zangu wawili wenye asili ya kiarabu. kwani mama yangu yeye pia ana asili ya kiarabu..... Ninae dada yangu ambae ana umri wa miaka 25 huyo ni wa kwanza na keshamaliza shule muda tu... kisha ninae dada yangu mwingine ambae tumefuatana.. yeye ana umri wa miaka 22 na yeye bado yupo kidato cha 4... afu anafatiwa na mimi kidume sharbiny rashidy mwenye umri wa miaka 20 na yupo kidato cha 3.... familia yetu ilikua ni familia ya kitajiri sana yaani tulikua ni matajiri waliopindukia.... Ila katika watoto wote wa mzee rashidy mimi peke yangu ndio nilikua nina rangi tofauti na dada zangu wote. Ila nyumba yetu imezungukwa na wafanyakazi wengi mno. kama kwa raisi vile kumbe ni kwa mtu tu wa ka...