MADAM BOSS
Sehemu Ya 2
Mtunzi..... Mgosingwa
Simu No. +255714419487 WhatsApp
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/
Ilipoishia Jana...........
SEKRETARI WA BOSI
"mwalimu.... Mbona unalia kuna nini tena.... Leo nina furaha juu ya matoke yangu,... Eti mama,... Kwani wewe huna furaha.... Mbona mwalimu analia"
Jafari aliongea maneno mengi sana lakini hajui nini kitamsibu.....
"jafari... Sio kuwa nalia kwakua sipendi ufaulu wako.... Ila sijui nitakuambia nini"
Maneno hayo ya mwalimu yalimfanya jafari nae kuanza kulia... Mama nae hakuchelewa kama unavyojua machozi ya mwanamke hayachelewi...
"sina budi kukuficha jafari wangu.... Ukweli ni kwamba"
Jafari kuskia hivyo akajua basi hapa kuna tatizo, mana mwalimu huyo ndie aliemsomesha toka kidato cha kwanza mpaka kidato cha nne, sasa kuna maneno gani tena anayotaka kuongea mwalimu huyo..... Kila mmoja akatega sikio kwa makini sana ili kujua nini tatizo juu ya jafari
ENDELEA..........
Kweli wapo watu wanaojitolea kumsaidia mtu kwa moyo mmoja, lakini, lakini pia wapo watu waliojitolea kumharibia mtu kwa moyo mmoja,.. Mwalimu jamali alipenda sana kumsaidia jafari mpaka mwisho wa masomo yake mana ni kijana anaejali masomo, hataki mchezo kabisa, lakini alitokea tajiri mmoja alioweza kuidhurumu haki ya jafari....
Mwalimu jamali alimwambia mama yake jafari kuwa kwa wakati huo hawezi tena kumsaidia jafari, kwasababu ana watoto wanaingia sekondari, hivyo Hatoweza kumhudumia jafari tena, japo kutoka kidato cha Kwanza ni yeye lakini kwa hapa basi ilitosha... Jafari alilia sana huku mama pia hakuacha kulia, mana ndio msaada pekee kwa jafari, sasa kama ataacha je jafari atasaidiwa na nani.... Basi mama na mtoto wake waliondoka baada ya kupewa ukweli kuwa mwalimu hawezi tena kumsaidia jafari hivyo watafute njia nyingine.....
HAPA SASA NDIO MWISHO WA KUMBUKUMBU YA MWALIMU JAMALI KABLA YA JAMALI NA MAMA YAKE KUFIKA SHULENI
Sasa hapa mwalimu jamali anamuona mzee tajiri anakuja tena kwa mara ya pili,... Anakuja kuchukuwa majibu kama kakubali au laaa..... Lakini mwalimu jamali akawaza mbali sana, kuwa achukue hio pesa kisha auze jina la jafari, halafu hio hio pesa ikanunue nafasi nyingine katika shule nyingine ili jafari aendelee kusoma... Hayo ndio mawazo ya mwalimu jamali.....
Tajiri aliingia na kukuta taarifa njema toka kwa mwalimu, lakini kukubali kwa mwalimu huyo ni kutishiwa kwenda kusingiziwa kuwa kamtia mimba mwanafunzi wake hivyo achukuliwe hatua kali,... Na tajiri kweli akiamua kufanya lake, utampenda mwenyewe, kwani yupo tayari kuharibu pesa kwa ajili ya mtu, tena masikini asie na mbele wala nyuma, ni ili kumkomoa tu
Tajiri huyo aliongeza mpaka pesa ili kazi yake ifanyike vizuri zaidi
"hakikisha mtoto wangu anapata hio nafasi... Mana nataka nimpeleke International school, sasa kwa sifa alionayo kwa sasa, haifai kumpeleka"
"sawa boss nitafanya kila liwezekanalo mtoto wako akasome huko"
"sawa, nakuachia hio kazi.... Tena nakuongeza na hela kidogo... Piga kazi sawa"
"sawa boss"
Tajiri huyo aliondoka zake na kuacha vumbi tu hapo shuleni,... Wakati huo mwalimu anahesabu pesa anakutana na milioni kumi taslimu...
"lazima jafari asome"
Aliongea mwalimu huyo kwasababu alipenda sana kumsomesha jafari kwasababu ni kijana mwenye heshima na mpenda masomo....
Mwalimu jamali alikwenda kuharibu nafasi ya jafari kuwa ya kumi kutoka mwisho na wa kumi kuwa wa pili kutoka mwisho,... Alikwenda kule kule NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA (NECTA) akaikanseli nafasi ya jafari na kuweka nafasi ya mtoto wa tajiri... Alihonga wafanyakazi walioandaa matokeo hayo kisha ikaanza kusomeka hivyo.... Jambo likawa limewezekana na jafari sasa yupo nafasi ya kumi kutoka mwisho, kwahio kama walikuwa wanafunzi mia moja, basi yeye ni mtu wa 90,... Inauma sana pale tajiri anapoamua mambo yake,.....
Lakini mwalimu jamali hakuishia kuharibu nafasi ya jafari, bali alianza kuzunguka katika shule mbalimbali ili jafari apate nafasi katika shule nyingine,... Mana hatamani kumpotezea nafasi hio kabisa.... Lakini pamoja na mwalimu huyo kujitahidi kutafuta shule aligonga mwamba, kwani kila shule inataka mwanafunzi awe na ufaulu mzuri ndipo iruhusu kumkubalia
"lakini mwanafunzi yupo vizuri mkuu"
Aliongea mwalimu jamali kumwambia mkuu wa shule aliofikia
"mwanafunzi yupo vizuri wakati kashika nafasi ya 90...yaani ni mtu wa kumi kutoka mwisho... Huyu hakuna shule itampokea kabisa.. Hata za kayumba huyu haendi....labda uhonge sana tena kwenye shule binafsi"
"mkuu, huyu mtoto ana akili sana tena sana"
Aliongea jamali huku akizidi kumzibitishia mtoto ana akili sana
"sasa utanielezaje kwa mdomo wakati max zake zinaonekana wazi wazi... Mtu ana nafasi ya kumi kutoka mwisho afu useme yupo vizuri,... Hebu usinipotezee muda mimi"
Mwalimu jamali aliendelea kutafuta shule, lakini kila shule majibu ni yale yale, mana kumruhusu mwanafunzi aanze kidato cha tano kwa kiwango cha nafsi hio, haiwezekani... Ni kuiabisha shule... Mwalimu jamali alikata tamaa kabisa mana kuzunguka jiji zima lenye shule bora lakini wapi hajapa...
"jafari, Utanisamehe mwanangu... Nilitegemea kupata shule lakini nimekosa... Nisamehe sana mwanafunzi wangu"
Mwalimu jamali alijiongelea mwenyewe akiwa chumbani kwake, baada ya kuchoka sana kwa kutafuta shule, na shule zote hazitaki mwanafunzi mwenye ufaulu wa hali hio,.... Mtu wa kumi kutoka mwisho hawezi kupata shule popote pale.. Basi mwalimu jamali hakupata shule kabisa na elimu ya jafari ndio imeishia hapo,... Yaani hapo ndio hakuna kuendeleza tena....
Jafari akiwa sokoni anachukua matunda na mboga mboga kwa ajili ya kibanda cha mama yake,... Aliona bora amsaidie mama yake kwenda sokoni mana hakuna jinsi tena... Shule ndio keshakosa hivyo hakuna cha ziada, mama hana uwezo wa kumsomesha mtoto... Mana shule itahitajika ada, mama hana kazi ya kuweza kumlipia mama.. Na atakwenda kumuomba nani...
"we mama, hizi nyanya zimelegea sana hizi... Nichagulie zingine"
Aliongea jafari wakati huo hana wasiwasi tena na hapo hajui kama nafasi yake imebadilishwa, kana kwamba akiona kwa sasa atashangaa sana...
"huyu mtoto wa mwajabu nae ana tabu huyu aaahh, haya shika na hizo"
"bado ngogwe... Afu na hoho weka"
"yaani nyie hicho kibanda chenu, balaa"
Aliongea mama wa sokoni ambae ndio anawauzia watu bidhaa za nyumbani, yaani kuna wale wamama ambao wana vibanda vya mboga mboga mtaani, miksa matunda, kila kitu,... Kama ulishawahi kuona kuna wale wamama wanatoka asubuhi sanaaa, na makapu yao makubwa kwenda sokoni, sasa hao ndio kazi ya mama yake jafari,... Lakini toka jafari ajue hana kwenda shule tena, aliamua kumsaidia mama yake kwenda sokoni....
"sasa ngoja nikachukue matunda na mananasi pale.... Afu hio pilipili hoho bovu ilo, weka vitu vyenye ubora bwana mama"
Aliongea jafari huku akielekea upande wa matunda,... Kapu lake lilijaa kila aina ya mboga mboga, viungo, matunda, kisha akapakiza kwenye baiskeli yake iliochakaa sana
"yaani mama Ashura, ningelipa mtoto kama huyu.. Sijui ningefurahi kiasi gani"
Aliongea mama mmoja alio uza matunda kwa jafari,...
"kweli huyu kijana anajituma haswa, afu naskia akili imelala hapo"
"yaani mimi nina mtoto wa kiume na wa kike... Yaani toto kila siku mtaani sjui kijiweni halina hata msaada, huyo wa kike sasa kila saa yupo na simu anapangusa pangusa namna hii... Yaani hawa watoto basi tena... Ila mtoto ni wa kiume lakini kaja kumsaidia mama yake"
Aliongea mama huyo kwa kumpa sifa jafari ama Jeff,...
"na uhensamu wake sasa, wala hajali"
"uhensamu mbele ya mama... Lazima ufanye kazi"
"afu sasa ni huyo huyo tu masikini ya mungu"
"alaaaaa, ivi mama Jeff hana mtoto mwingine"
"hana... Yeye anasema wala hatamani kuona jidume linamsogelea, anakwambia toka ajifungue huyu Jeff wake hajui mwanaume alivyo mpaka leo na umri ule"
"aaaahhh sasa kwanini"
"alitendwa yeye mwenyewe ndio kasema"
Basi yalikuwa ni maneno ya wamama hao lakini wakati huo jafari yupo njiani na baiskeli yake iliojaa kapu la mboga mboga,...
Mama kumuona mtoto wake anakuja huku akikokota baiskeli na mzigo juu ya baiskeli... Mama alimkimbilia mtoto wake
"mbona unakokota umefanya nini"
Aliuliza mama yake jafari huku jafari akijibu kuwa
"naona ni pancha hii... Mana niliskia tu pwaaaaaaaa"
"oooohhh pole sana baba... Lete nikusaidie"
"we mama wewe.. Unataka kuumia sasa si ndio eee"
"we lete... Mimi nilikuwa nabeba toka ukiwa mdogo... Unashangaa leo"
"weeee mama subiri utaumia mama angu.. Kuwa mpole, kama ulibeba na baiskeli ni miaka hio.. Sasa hivi mimi nipo kaaa chonjo mama, ni zamu yangu kubeba"
Aliongea jafari huku mama akitabasamu tu, mana ana dume la nguvu, ila mama akikumbuka elimu ya mtoto wake,.. Anaumia roho sana
"haya, toa sasa kwa utaratibu... Afu wenzako wabaya wale.. Walikuwa wananipa nyanya mbooovu... Aisee wale tuwahame nini"
Aliongea adam huku mama akipakua mboga kutoka kwenye baiskeli...
"hapana usiwahame, nimeanza nao muda mrefu sana"
Mama alimaliza kushusha mboga na matunda kisha jafari akasema kuwa
"mama... Ngoja nilipeleke hili fuso kwa fundi"
"sasa una hela... "
"ahhh fundi rafiki yangu yule"
"hapana bwana, shika hii elfu moja.. Ukazibe hio pancha"
"mama... Kaa nayo hio elfu moja itatusaidia mambo mengine"
Aliongea jafari huku akiondoka kuelekea kijiweni....,
"basi usichelewe baba... Leo napika ubwabwa ujue"
"aahhhhh mamaa... Chakula changu hicho"
"najua, sasa ole wako uchelewe"
"najua hata nikichelewe huezi nimalizia"
"mshenzi wewe, kwenda uko"
Basi ilikuwa ni furaha ya mama na mtoto,.. Ama kweli mtoto kwa mama hakui, na ndivyo ilivyo kwa jafari....
Jafari alifika kijiweni kwa kaka yake wa mtaani,
"aaahh kaka kaka naona upo bwana"
"aaahhh dogo vipi.... Mbona gari yako imebonyea"
"aahhhh nimetoka sokoni jioni hii.. Kuchukua bidhaa kwa ajili ya kesho bandani, sasa nikaskia tu pwaaaaa.. Nikajua kimenuka hicho"
"haya sasa binua gari, si unajua kutengeneza"
"aaahhhhh kakaaaa mimi sio wa kiivyo... We ngoja uone vitu vyangu"
Jafari aliibinua baiskeli yake miguu juu kisha akaanza kuifungua ili aitengeneze bure mana ni kwa kaka yake wa mtaani... Ikiwa ni majira kama ya saa 12 hivi za jioni...
Huku nyumbani mama alikuwa anapanga vitu katika kibanda chake, mana vibanda vya mtaani vinauza mpaka usiku, tofauti na sokoni mwisho saa 12 jioni... Mama anapanga nyanya vizuri... Tena wakati huo mama napanga huku anaimba nyimbo fulani hivi ya warumba chee...
"ningekuwa kweeetuuuu, ningekuwa kwetu... kwetu ni umbali ningemlilia mamaaa"
Mama nyimbo hio aliipenda sana kuiimba sasa sijui ana maana gani.. Lakini akiwa anaendelea kuimba.. Ghafla alishtuliwa na suti ya honi ya gari....
"pwiiiii pwiiiii"
Mama kuangalia mbele.... Laaaa haulaaa , ni bongo la gari tena la gharama kubwa.... Mama jafari akahisi labda sio yeye,... Mana hata hata rafiki mwenye gari, sasa haoni haja kuhangaisha sikio lake kwenye magari... Mama akaendelea kuimba nyimbo yake...
"ningekuwa kweeetuuuu, Oieee ningekuwa kwetu.... Kwetu ni umbali ningemlilia mamaaa"
Aliimba mama huyo huku akipanga matunda yake... Ghafla alishtuliwa na sauti
"nyimbo nzuri, ila kwanini hupo makini na biashara"
Ilikuwa ni sauti ya kike tena ilio nyororo haswa... Mama akainua shingo yake kumtazama anaemuongelesha..... Haaaa,..... Laaaaaa haulaaaaaa,... Mama haamini macho yake..
GHARAMA YANGU NI SHARE 200 TU,
ZITAKAPOFIKA TU, NAENDELEZA...
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/
STORI ZANGU ZOTE HIZI HAPA....
(1).KIJAKAZI WA KIUME
(2).MLINZI WA GETI
(3).DEREVA TOYO
(4).MTOTO WA HAYATI
(5).ONE DAY YES
(6).SECONDARY SCHOOL
(7).FUNDI CHEREHANI
(8).MWIGIZAJI BALAYA
(9).THE DOM
(10).THE ISLAMIC WIFE
(11).MKE JEURI
(12).YOUNG PASTOR
(13).MUUZA CHIPSI
(14).WAPANGAJI WENZANGU
(15).NYAMA YA MAMA
(16).MADAM BOSS
KUZISOMA ZOTE, BONYEZA HAPA
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/
AU.... NICHEKI KUPITIA NAMBA +255714419487 WhatsApp
Utazipata Zote Mpaka Mwisho Kwa Simu No: +255714419487 WhatsApp, Au, Like Page Yetu Ya Facebook Kwa Kubonyeza Hapa Chini ili Usipitwe
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/
tAfBoy {.Tanzania's Frugal Boy..}

Comments
Post a Comment