Skip to main content

WAPANGAJI WENZANGU Sehemu ya 1

WAPANGAJI WENZANGU

Sehemu Ya 1

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/

Inapoanzia Rasmi...

FUNDI UJENZI

Simulizi yetu inaanzia katika jengo moja ambalo lilikuwa likijengwa,.. (SITE) palikuwa na wafanyakazi wengi sana hususan mafundi na wasaidizi pamoja na wakandarasi wenyewe,... Ikiwa ni siku ya Jumamosi nyakati za jioni,.. Ni ile siku ya malipo kwa wajenzi,... Walikuwapo wafanyakazi wengi sana tena wa jinsia tofauti, hata wanawake nao walikuwa wakionekana katika kazi hizo kwani hali ni ngumu hata wanawake wanapiga zege kama wanaume, mana hawapati wanaume wa kuwaletea nyumbani hivyo wameona ni bora kuzifuata huko huko zinako toka...

Madaftari ya kusaini pesa yako mawili, yaani daftari la mafundi na daftari la wasaidizi,... Mafundi walilipwa elfu ishirini na tano kwa siku, hivyo kwa wiki anatakiwa kusaini shilingi laki moja na hamsini (150,000), kwa wiki.... Lakini pia kuna wasaidizi wao,.. Wao daftari lao husaini shilingi elfu kumi tu kwa siku, hivyo kwa wiki atatakiwa kusaini shilingi elfu sitini (60,000) kwa wiki hivyo sio pesa mbaya sana hata kama una familia maisha yanakwenda



Baada ya malipo kila mmoja alisambaratika na kwenda makwao, lakini kuna fundi mmoja aliokwenda kwa jina la HASSAN, ana vijana wake wasiopungua wanne,.. SWALEHE, JEREMIAH, ABEDI, MAHMUD, hawa vijana wote wanaishi chumba kimoja pamoja na huyu fundi,... Kwahio chumba kimoja wanalala watu watano,.. Maisha ya mjini ya kutafuta pesa, usione ajabu hata watu kumi kulala chumba kimoja,... Kila mmoja anajipanga kivyake...

Lakini watu hawa watano wakiwa na fundi wao na pia ni kaka yao ambae amewapokea na kuwahifadhi, japo kila mmoja kaja kivyake au kakutana na Hasan kivyake na kamlalamikia kivyake,.. Hasan mpaka sasa hana mke, na yote hio huenda ni kwasababu anaishi na vijana wengi sana katika chumba kimoja...

"sasa madogo?, wacheni nikashtue kidogo"
Aliongea fundi Hasan, huku na wale wakushtua kama yeye wakimuunga mkono,..
"aisee hata mimi nina hamu na demu, daahh wacha niende bondeni"
Alionge jelemia huku Abedi na fundi hasan wakielekea baa kutoa loku (kunywa pombe).. Lakini wapo vijana wawili wao hawakuwa watu wa starehe kama walivyo wenzao ambao kila mmoja kataamka starehe yake
"asee swai, kama kawa basi nenda na zana zetu"
Aliongea hasan huku wakimkabidhi swalehe na Mahmud zana ambazo wametoka nazo kazini, mana wao hawafiki nyumbani kwa wakati huo, kwakua swalehe na Mahmud wao hawana starehe yeyote ile, walichukua zana za wenzao na kuondoka kurudi nyumbani....
"aisee tukute vyombo vimeoshwa ee"
Aliongea abedi huku swalehe akiitikia
"sawa ndugu"
"ah ah, nawe unaitikia tu, kwani we ni mke wao"
Alionge Mahmud au mudi, huku swalehe au swai akijibu
"sasa tutafanya nini... Tupo kwenye geto la watu, hivyo lazima tuende sawa"
Aliongea swalehe huku Mudi akimuuliza
"wewe una muda gani hapa mjini"
"miaka kumi"
"sasa miaka yote hio hujajipanga tu"
Aliongea mudi huku swai akijibu
"sio miaka yote nilikuwa na kazi... Nina miaka mitatu kwenye kazi hii na bado sijawa fundi"
Aliongea swai huku wakirudi nyumbani na hapo kila mmoja kabeba begi la mwenzake ambae kaenda baa,
"lakini hasan si ndugu yako kabisa wewe"
"ndio,... Baba mmoja mama mbalimbali"
Alijibu swalehe huku mudi akizidi kumuuliza
"kwahio miaka yote kumi unaishi nae tu"
"kama kawaida"
"duuuuuuu, una moyo... Kuishi miaka kumi geto afu mpaka sasa huna kitu"
"skia mudi... Mimi nilikuwa sina kazi... Miaka mitatu iliopita ndio broo akaniambia, twende ukawe saidia fundi, na mpaka sasa hata ufundi naweza"
Aliongea swalehe ambae ni ndugu yake na hasan, kwahio swalehe na hasan ni ndugu, lakini Abedi, mudi, na jelemia wao wamepewa hifadhi tu kama walivyo omba wahifadhiwe mpaka watakapo pata pesa ya kujipangishia vyumba vyao
"sasa kwanini usiwe fundi"
"namwambiaga ujue... Lakini yeye ananitishia eti ooohh ufundi sio ishu ya mchezo... Utakuja kutia hasara ujenge nyumba mara ibomoke, sjui nitafungwa... Mambo mengi ndio mana nimetulia tu"
"ah ayo matisho tu"
"ni sawa lakini ni mkubwa wangu ujue"
"kwahio unaogopa ile ASIESIKIA LA MKUU HUVUNJIKA GUU"
"haswaaaaaaaa"
"hahahahahahahahahha.... Ila swai tuongee na kurudi nyuma... Muda ulio ishi kwa kaka yako.. Ni mkubwa sana,... Fanya hima uachane nae"
Aliongea mudi kama kumshauri swalehe
"wazo lako mudi, ni zuri sana... Lakini umechelewa"
Aliongea swai huku akicheka kwa kujinadi
"kwanini nimechelewa"
"huuu ni mwezi wa ngapi huu"
"wa kwanza"
"sasa wa pili mwishoni nahama kwa broo..."
Aliongea swalehe huku mudi akiwa haamini
"acha utani wako"
"aaaaaaaaaa.... Na pia nina maana ya kusema mwezi wa pili... Kwasababu nilikuja Arusha rasmi tarehe 28 mwezi wa pili, sasa nataka niondoke tarehe hio hio mwezi wa pili.. Kwahio mwaka huu mwezi wa pili ndio natimiza miaka kumi kukaa kwa broo... Ila mwezi wa pili sipo"
"duuuuu umejikomboa wewe... Sisi bado tutabanana na broo wetu"
Aliongea mudi huku swalehe akimwambia
"lakini hata wewe una uwezo wa kujipanga ujue"
"ni kweli, na sio mimi tu.. Hata akina abedi na jelemia wote tuna uwezo ila tumeamua kuvuta nguvu kiasi"
Aliongea mudu huku akikumbuka starehe yake....
"ayaaaani, afu nilikuwa napapita eti... Swai una stori za ajabu mpaka napita chakula ya baba"
Aliongea mudi huku akirudi nyuma, kununua starehe yake,... Kumbe mudi yeye ni mzee wa bangi... Hapa bado swalehe ndio hatujajua starehe yake
"nishkie begi"
"nani ashike... Twende uko uko"
Alionge swai huku akienda nae kwa pusha kununua bangi,... Kama kawaida kwa pusha hua kuna masela wengi sana kwasababu ndio chakula cha baba kilipo
"aaahhh swai... Mambo vp bwana"
"poa nambie"
"guda... Naona chalii yako kaja kuchukua chakula cha baba"
"eeehh kama kawaida yake mwenyewe"
Aliongea swai huku akiwa na masela nao wavuta bangi, lakini swalehe yeye havuti chochote kile... Ila anaishi na masela wavuta bangi na wanywa pombe lakini hakuwahi kushawishika kutumia kilevi chochote kile... Na anaishi nao nyumba moja...

Basi mudi alinunua stiki zake kadhaa, kisha wakawa wanarudi geto,.. Geto hapakuwa mbali sana, walifika wakiwa wamechoka mno,...
"huu umeme ndio umekata au luku"
Aliongea swalehe huku akiwasha washa taa,..
"itakuwa luku hii... Na kama ni luku, hapa ipo kazi ya kukamatana na wapangaji, mana mpaka watoe,... duuu"
Aliongea mudi huku akitandika kitanda mana asubuhi kila mtu anakurupuka na njia yake, japo kazi yao ni moja laki hakuna anaekumbuka kutandika asubuhi, na hapo ndani kuna vitanda viwiliwili, uzuri chumba wanacho ishi ni kikubwa na kimeenea vitanda viwili vya nne kwa sita...
"aisee kama umeme umekata wataniua sasa"
Aliongea swalehe huku mudi akicheka
"ehehehehehehe najua wataka kuchati.... Na huo ndio ugonjwa wako swai... Yaani ukishika huo mtachi wako hutoki"
"mbona we ukivuta bangi lako unalegeza macho"
"basi yaishe... Sasa kabla hujashika hio simu yako... Kwanza tufanye mchakato wa kula... Mi naosha vyombo, we anza kuchambua dagaa"
Aliongea mudi kama kupeana kazi
"anza sasa... Mimi nikimaliza nabadika safuria"
Aliongea swai huku kila mmoja akishika nafasi yake ya kazi mana wao wawili tu ndio wamerudi nyumbani, wengine wameenda kulewa
"tupikie makamanda"
"kawaida tu"

Kesho yake ikiwa ni siku ya Jumapili, mida ya saa mbili asubuhi lakini masela walikuwa bado wamelala mana hakuna pa kwenda siku hio,.. Lakini swai yeye alikuwa bize na simu kana kwamba swalehe starehe yake ni kuchati tu, yaani usiombe simu ikakuingia damuni,.. Yaani kama akili huna hata kwenye kazi utakuwa mvivu, ila swai kwenye kazi anafanya kazi lakini akiwa free, humsumbui kwenda popote,.. Hata ukampe ofa ya nini.. Hataki labda simu iishe chaji na hakuna umeme...
"oya fanyeni mpango wa chai basi"
Aliongea hasani huku vijana wakiamka kufanya alicho kisema hasan, mana ndio mkubwa wao na ndio fundi wao na ndio geto kwake, hivyo hawana ubishi juu yake,...

 Baada ya masaa saba wakiwa wanakula chakula cha mchana ili kila mmoja asambaratike na Jumapili yake,... Lakini hasani leo kuna jambo alitaka kuwaeleza vijana wote ambao anaishi nao
"oya... Mtu wa mwisho kumpokea kwangu ana miaka miwili hapa geto... Ni kweli si kweli"
Aliongea hasani huku wote wakisema
"ni kweli broo"
"sasa ni hivi... Najua baadhi yanu tumefanya starehe sana.. Ila kama hujajipanga utajua mwenyewe... Sasa hivi nataka kuoa... Kwahio nawapa wiki hiii.. Moja tu, kila mtu apangishe chumba chake"
Aliongea hasani huku baadhi ya vijana wakishika vichwa, mana walikuwa wakila maisha tu..
"sasa broo, mbona umetushtukiza hivi"
Aliongea abedi huku hata kula hana hamu
"nawapa wiki moja tu... Na ndio mana nikasema leo... Mana kama nikisema hio siku mtaniona mbaya mjue"
Aliongea hasani huku swalehe akitabasamu tu mana wazo analotoa lipo akilini mwake... Vijana wengi walilalamika haswa wale wapenda starehe mana hawaja jiwekea hata pesa ya godoro...
"broo... Mi naona ungetupa mwezi mmoja, kwasababu wengu wao hapa hawapo vizuri mifukoni mwao"
Aliongea swalehe, lakini yeye aliongea kama kuwatetea wenzake, na pia yeye mwenyewe ana uwezo wa kuondoka hata siku hio, lakini kajiwekea tarehe ya kuondoka kwa kaka yake,..
"wewe unasema wao je wewe"
Hasan alimuuliza mdogo wake
"broo, mimi hata kesho naweza kuondoka... Lakini nina tarehe maalumu ya kuondoka"
"kwahio upo vizuri"
"ndio.. Tena natoka na nguo zangu tu"
"kitanda chako hiki"
"atachukua mudi"
"na wewe"
Hasan alimshangaa sana mdogo wake mana kitanda kimoja hapo ndani ni cha swalehe, lakini hakihitaji
"broo, nimekaa sana kwako, hivyo sitaki nipangishe chumba na vitu vya zamani... Nataka vitu vipyaaaa, tena vya maana.."
Aliongea swalehe huku abedi akisema
"duuuuu Afadhali wewe swai... Mana mimi hata huo mwezi mmoja haunitoshi"
Aliongea abedi huku jelemia nae akisapoti
"aisee ni kweli hata mimi huo mwezi haunitoshi"
"nyoooooo.... Hapa nawapa huo mwezi tu,.. Kama mtu hawezi atajua mwenyewe, nataka kuoa bwana.. Nimesema hivi nawapata huo mwezi mmoja tu... Ukiisha huu mwezi wa pili sitaki kuona mtu..."
Aliongea hasani kisha akanawa mikono na kuondoka zake
"aaaaahh.... Sasa itakuwaje... Aisee swalehe, pangisha basi tuje kuishi"
Aliongea jelemia huku swalehe akijibu
"weeeeeee, kwanza hata mimi nikipangisha naoa... Staki kukaa na mtu sawa.. Labda mumwambie mudi"
SWALEHE alikataa kuishi na mtu mana wao walikuwa wakifurahia maisha bila kujua kuwa kuna maisha baada ya kifukuzwa kwa mtu
"ah ah swai... Usiwaelekeze kwangu.. Kwani mimi sitaki kuoa... Hata mimi jamani nataka kuoa... Nyie pesa zenu mnapelekea malaya na pombe, haya nendeni mkalalie huko"
Aliongea mudi ambaye yeye starehe yake ni bangi tu basi..... Swalehe aliondoka zake na wengine kila mmoja aliondoka zake mana siku hio ni siku ya Jumapili

BAADA YA WIKI MBILI KUPITA

Swalehe alikutana na dalali mmoja ili ampe kazi ya kumtafutia chumba,..
"sasa skia mzee,.. Mimi nataka chumba kizuri, kwanza kiwe na maji ndani, kiwe na umeme"
Aliongea swai huku dalali akiwa na maneno mengi
"aaahh hapa umefika... Yaani hapa utapata chumba cha aiana yeyote... kwanza kuna chumba kimoja hapo mtaa wa pili ebu twende"
"wapi apo"
"hapo mnarani"
"aaahh mzee mimi siwezi kwenda kuishi ungalimitedi bwana.."
"ah ah sio ungalimitedi kijana.. We twende, kwanza chumba kizuri"
Aliongea mzee huyo huku swai akiamka na kumchukua mzee wakakione hicho chumba, wakati huo swai kavalia nguo zake za kazi,..

"geti hili hapa... Umeona kwanza geti lenyewe kali,... Haya twende ndani"
Aliongea dalali huyo huku wakiingia ndani,... Kwanza kufika tu wakaona wamama wamekaa vibarazani mwao,
"umeona, nyumba imechangamka hii, hata mkeo hatokuwa na tabu"
Aliongea mzee huyo ambaye ni dalali
"nionyeshe chumba mzee, acha maneno"
"sasa chaguo ni lako... Unataka dabo rumu au singo rumu"
Aliongea dalali mana hapo kwenye hilo boma kuna pande mbili, kuna upande wa dabo rumu na upande wa singo rumu... Na inaonekana watu wamehama muda sio mrefu...
"hawa wamehama kwasababu gani"
Aliuliza swai huku mzee akijibu
"mimi sijui.. Ila angalia chumba saafi,.. Maji yale pale... Umeme huoooo"
"mmmhhh kuna wamama humu duuuuu"
"ukiona nyumba ina wanawake wengi, ujue ina amani hio"
"mmmmhhhhh, wana vilanga hao"
"weeeee ongea taratibu ukisikiwa.."
Aliongea dalali huku swalehe akiuliza mama mwenye nyumba...
"mama mwenye nyumba yupo wapi"
"hapa tutamfuata baba mwenye nyumba ndio kila kitu..."
"sawa yuko wapi"
"yeye anaishi nyumba ya pili huku"
"ok twende"
"lakini umekipenda chumba hicho"
"we twende kwa mwenye nyumba"
Aliongea swalehe mana kakutana na dalali ana maneno mengi sana... Lakini sasa ile wanatoka tu.. Mara dalali kaitwa na wamama waliokuwa wamekaa vibarazani
"we mzee jumbe njoo hapa"
Wamama walimuita dalali huyo
"enhee mnasemaje, kuna mtu anataka kuhama kati yenu?... Vyumba vipo ni nyie tuuuu"
Aliongea dalali huku wapangaji wakaanza kusema
"hatuna shida na kuhama sisi... Hivi wewe dalali, unaona hii hadhi ya hii nyumba"
"ndio"
"umemuona yule anaepangisha hiki chumba"
"yule kijana au nani"
"ndio, yule mwenye kofia kama muuza nyanya"
"kwani kuna nini jamani"
Wakati huo swai katulia pembeni na anasikia kwa mbaaali
"hivi yule na kofia lile, na mandevu yale... Mchafu vile, aje apangishe humu"
Aliongea Madada mmoja au mama fulani.. Wakati huo swai kasimama nje ya geti akimsubiri dalali aje waende kwa baba mwenye nyumba, lakini ghafla swai anashikwa bega huku akisikia
"nyie ndio wezi ninao watafuta... Haya niambie unachungulia nini huku ndani... Umeona nini cha kuja kuiba?"
Alikuwa ni mzee mmoja wa makamo akiwa kamshika swai,..
"hapana mzee nimekuj"
"tuliaaaaa... Hapa umeingia kwenye mikono ya jeshi,.. Mimi ndio mzee zubery mwanajeshi mstaafu.... Kaa chini haraka"

GHARAMA YANGU NI SHARE 200 TU,
ZITAKAPOFIKA TU, NAENDELEZA...

www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/

STORI ZANGU ZOTE HIZI HAPA....

(1).KIJAKAZI WA KIUME

(2).MLINZI WA GETI

(3).DEREVA TOYO

(4).MTOTO WA HAYATI

(5).ONE DAY YES

(6).SECONDARY SCHOOL

(7).FUNDI CHEREHANI

(8).MWIGIZAJI BALAYA

(9).THE DOM

(10).THE ISLAMIC WIFE

(11).MKE JEURI

(12).YOUNG PASTOR

(13).MUUZA CHIPSI

(14).WAPANGAJI WENZANGU

KUZISOMA ZOTE, BONYEZA HAPA
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/

AU.... NICHEKI KUPITIA NAMBA +255714419487 WhatsApp

Utazipata Zote Mpaka Mwisho Kwa Simu No: +255714419487 WhatsApp, Au, Like Page Yetu Ya Facebook Kwa Kubonyeza Hapa Chini ili Usipitwe
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/

tAfBoy {.Tanzania's Frugal Boy..}

Comments

Popular posts from this blog

JAMANI ANKO Sehemu Ya 1

JAMANI ANKO Sehemu Ya 1 MTUNZI: George Iron Mosenya SIMU:0655727325 Nilitamani muda wa vipindi darasani umalizike ili iweze kutimiza ahadi niliyokuwa naisubiri kwa siku nyingi. Mwalimu alikuwa akifundisha lakini ni kama nilikuwa sielewi wala sisikii alichokuwa anaelezea. Mawazo yangu yote yalikuwa kwa Madam Jesca. Siku hiyo nilijisemea kuwa iwe isiwe lazima nimweleze ukweli na ikibidi siku hiyo hiyo yatimie ninayoyawaza kila kukicha. Madam Jesca alikuwa ni mwalimu aliyekuwa akitufundisha kwa muda tu baada ya kuwa amemaliza kidato cha sita. Wakati huo sisi tulikuwa kidato cha nne. Somo alilokuwa akitufundisha ni Kiswahili. Hatimaye mwalimu akatoka na baada ya nusu saa nikaondoka kuelekea nyumbani kwa madam Jesca. Niliingia baada ya kuwa nimegonga hodi. “We Joshua mbona muda wa vipindi hivi we umekuja huku..” aliniuliza huku macho yake yakionyesha mshangao wa waziwazi. Kanga yake aliyovaa ilikuwa imelowana na hivyo kusababisha niuone mstari wa chupi. Na kama hiyo haitoshi madam Jesca...

SECONDARY SCHOOL Sehemu Ya 1

SECONDARY SCHOOL Sehemu Ya 1 Mtunzi..... MoonBoy Simu No. +255714419487 WhatsApp Inapoanzia Rasmiiii STORY HII INAITWA SECONDARY SCHOOL AU KWA KISWAHILI NI ( SHULE YA UPILI )..... KWAHIO PIA WAWEZA KUIITA HIVYO TU BASI Story hiii mimi ni mtoto wa kitajiri ile mbaya... na wakiume nipo mimi mwenyewe na nina dada zangu wawili wenye asili ya kiarabu. kwani mama yangu yeye pia ana asili ya kiarabu..... Ninae dada yangu ambae ana umri wa miaka 25 huyo ni wa kwanza na keshamaliza shule muda tu... kisha ninae dada yangu mwingine ambae tumefuatana.. yeye ana umri wa miaka 22 na yeye bado yupo kidato cha 4... afu anafatiwa na mimi kidume sharbiny rashidy mwenye umri wa miaka 20 na yupo kidato cha 3.... familia yetu ilikua ni familia ya kitajiri sana yaani tulikua ni matajiri waliopindukia.... Ila katika watoto wote wa mzee rashidy mimi peke yangu ndio nilikua nina rangi tofauti na dada zangu wote. Ila nyumba yetu imezungukwa na wafanyakazi wengi mno. kama kwa raisi vile kumbe ni kwa mtu tu wa ka...

MUUZA CHIPSI Sehemu Ya 1

MUUZA CHIPSI (MKE WA KAKA) Sehemu Ya 1 Mtunzi..... MoonBoy Simu No. +255714419487 WhatsApp www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/ INAPOANZIA RASMIIII Jamani Simulizi hii, sio moja, bali zipo simulizi mbili ndani ya moja... Kuna simulizi yangu moja iliitwa MKE WA KAKA hio simulizi inaendana na simulizi hii ya MUUZA CHIPSI, hivyo sikutaka simulizi zangu ziwe zinajirudia, hivyo nimeiweka sehemu moja zote mbili, mana stori za simulizi hizi zinaenda.. Hivyo ukisoma jua kua unasoma simulizi mbili ndani ya moja... Ila simulizi halisi ni MUUZA CHIPSI ikifuatiwa na MKE WA KAKA ambayo nayo ipo humu humu ndani,.   Na utaijua hapo itakapoanzia rasmi lakini mwanzo wa zote ndio, lakini pia MKE WA KAKA ina mwanzo wake huko mbele, hivyo nayo inaanzia hapa hapa....... Sasa ole wako uikose staki maswali mengi mana umekosa uhondo mwenyewe... Hivyo msije mkashangaa mke wa kaka kawa MUUZA CHIPSI.... ______________________________________ MUUZA CHIPSI Ni simulizi inay...